0
Mganga aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai mazito kuwa ndiye aliyemng’arisha staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ hivyo
kutoa siri nzito ambayo wengi hawakuijua.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mganga huyo amekuwa akimfanyia ndumba msanii huyo ili arudiane na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul
‘Diamond Platinum’.

Staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah
Abdukareem ‘Meninah La diva’.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mganga huyo amekuwa akidai kwamba, huwa msanii huyo anatinga nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar kisha kumlilia shida yake akimtaka afanye juu chini kuhakikisha anamrudisha Diamond mikononi
mwake.

Baada ya kukisikia chanzo hicho, waandishi wetu walikwenda nyumbani kwa mganga huyo na walipomuuliza ishu hiyo alikiri Meninah kufika
kwake ili kufanyiwa ndumba arudiane na
Diamond.

Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ akipozi. “Yule msanii anayeitwa Meninah ambaye habari zilivuma kuwa anatoka na Diamond na kukanusha, huwa anakuja hapa kufuata tiba na
kikubwa anachokitaka anataka nimvute Diamond ili warudiane,” alisema.

Meninah alipoulizwa kuhusu madai hayo aliruka kimanga na kudai hakuwahi kuwa na uhusiano na Diamond na wala hamjui mganga huyo.

Chapisha Maoni

 
Top