0
Polisi wakirusha gesi za kutoa machozi dhidi ya Waandamanaji St Louis



Mji wa St Louis limeshuhudia maandamano na vitendo vya uporaji baada ya jaji kupitisha uamuzi
wa kumshtaki aliyemuua kijana mweusi Michael Brown.

Polisi mjini humo wamesema vurugu zimeleta madhara makubwa zaidi kuliko ya mwezi Agosti baada ya kuuawa kwa kijana huyo.

Kamanda wa Polisi wa St Louis, Jon Belmar amesema alisikia milio ya risasi takriban 150 kutoka kwenye makundi ya watu.
Brown alifyatuliwa risasi na Polisi tarehe 9 Mwezi Agosti, hali iliyoibua ghadhabu na maandamano. Watu wengi wa jamii ya Afrika na Marekani walitoa wito wakitaka Afisa Polisi Darren Wilson ashtakiwe kwa mauaji.

Rais wa Marekani Barack Obama alitoa wito kwa wamarekani kuwa watulivu na kukubali maamuzi ya Jaji kuhusu kesi hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top