0
Maafisa wa kijeshi nchini Mali wanasema kuwa
watu waliokuwa na silaha wamewateka nyara watoto kumi na kuwaua wawili ambao walijaribu kupinga kutekwa karibu na mji wa Kidal.

Afisa mmoja alisema kuwa watoto hao
walilazimishwa kuwa wanajeshi.

Maeneo yanayozunguka mji wa Kidal yanadhibitiwa na kundi la kiislamu lililojitenga ambalo lilidhibiti eneo la kaskazini nchini Mali mwaka 2012 lakini
baadaye likatimuliwa na wanajeshi wa Ufaransa kwa ushirikiano na vikosi vya muungano wa Afrika.

Chapisha Maoni

 
Top