Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza. Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo
wanatuhumu polisi kwa kufunga baadhi ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea vifo hivyo alihuzunika sana.
Chapisha Maoni