0
Waziri mkuu wa Japani, Shinzo Abe (kushoto), baada ya tangazo rasmi la kuvunjwa kwa Bunge la Japani,
Novemba 21 mwaka 2014.

Na RFI
Miaka miwili tu baada ya kuingia madarakani, Waziri mkuu wa Japani, Shinzo Abe, ameamua kuitisha kura
ya maoni ili raia watoe msimamo wao kuhusu msukumo mpya unaoendana na mpango wake kabambe wa kuimarisha uchumi wa Japani ambayo ni yatatu kwa uchumi duniani.

Shinzo Abe amekua akipendelea kuona ongezeko la pili katika mfumo wa VAT, ambao ni wa kwanza, na ulipelekea sekta ya uchumi nchini Japani kupiga
hatua ya kuridhisha.

Akiwa na udhaifu katika uongozi wake, Waziri mkuu Shinzo Abe, amekua akionekana kuwa ni mtu anayetaka kujitengenezea umaarufu, lakini raia wa
Japani hawaelewi kwa nini Shinzo Abe anaandaa uchaguzi mapema, utakaofanyika Desemba.

Waziri Mkuu Shinzo Abe amevunja Bunge miaka miwili kabla ya muda wake kukamilika, wakati ambapo chama chake kina Wabunge wengi. Shinzo
Abe amebaini kwamba amefanya hivo kuomba raia wa Japani iwapo watapitisha uamuzi wake wa kuongeza kwa mara ya pili mfumo wa VAT kutoka
asilimia 8 hadi asilimia 10.

Ongezeko la kwanza mwezi Aprili, kutoka asilimia 5 hadi asilimia 8, ulisababishwa na mdororo wa
kiuchumi, ikiwa ni mageuzi ya nne katika mfumo huo wa ongezeko la VAT tangu mwaka 2008. 

Kulingana na utafiti, asilimia 65 ya raia wa Japani hawaelewi kwa nini Shinzo Abe ameharakia kulivunja Bunge ili
aweze kukabiliana na mdororo wa kiuchumi kupitia mfumo wa VAT hadi mwaka 2017, wakati ambapo
upinzani umeanza kujidhatiti.

Shinzo Abe amesema kuwa uamuzi wowote kuhusu mfumo wa kodi una ushawishi mkubwa kwa maisha
ya raia, kwa hiyo kuna ulazima mfumo huo upitishwe kwa kupigiwa kura na raia, amesema Abe. 

Waziri mkuu amepanga kuanzisha mfumo mpya kabla ya kutekeleza mageuzi yasiyokuwa na umaarufu
kimuundo kama vile soko la ajira na kilimo. Upinzani unamtuhumu Waziri mkuu kutaka kupata muhula mpya wa miaka minne ili aweze kunyamazisha wakosoaji wake kabla ya kuanzisha
upya mitambo ya nyuklia ambayo ilifungwa tangu ilipotokea ajali ya Fukushima.

Chapisha Maoni

 
Top