0
Kombe la Shirikisho la Soka Afrika,
AFCON



Upangaji wa makundi ya timu kumi na
sita zilizofuzu kucheza fainali za
mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015
yamefanyika katika mji mkuu wa
Equatorial Guinea, Malabo.

Mashindano hayo yataanza Januari 17,
2015.
Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki
moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial
Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua
nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae
mashindano hayo, lakini ilishindwa
kufanya hivyo baada ya kutaka
mashindano hayo yasogezwe mbele
kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao
umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika
Magharibi, ambako zinatoka timu nyingi
zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya
timu kubwa zilizoshindwa kufuzu
kucheza fainali za mwakani, pamoja na
Misri na Angola ambazo zote kwa
mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON
2015:
Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso,
Gabon, Congo
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR
Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa,
Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon,
Guinea
Wenyeji Equatorial Guinea na Congo
zitacheza mechi ya ufunguzi wa
michuano hiyo. Kundi D ndilo
linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu zilizopangwa kundi hilo. 

Chapisha Maoni

 
Top