ni nani na nani au Chama kipi kimetusua kwa kufanya vyema Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014-2015, haya ndiyo yaliyobainika haraka kujiri kutoka mkoani Mwanza:-
*Taarifa ya kwanza ambayo siyo nzuri ni tukio la simanzi la Mgombea Uenyekiti mtaa wa Luchelele kata ya Luchelele kupitia CCM Pius Masome kufariki dunia ghafla wakati zoezi la upigaji kura
likiendelea.
Ilikuwa ni majira ya saa tano na dakika chache mara baada ya kupiga kura sasa ile wakati akitembelea kukagua vituo mbalimbali vya eneo la wapiga kura wake ghafla aliona kizunguzungu
akaanguka na kupoteza uhai.
*Vurugu za kundi la vijana waliokuwa
wamejipanga kuzuia wapiga kura eneo la ibanda kata ya Kirumba kwenye kituo cha Shule ya Msingi Ibanda kata ya Kirumba kwenye kituo cha shule ya Msingi Ibanda walitawanywa kwa
mabomu ya machozi majira ya saa 7:00 mchana na askari wa kutuliza ghasia FFU.
*Katika kata ya Mahina mtaa wa Mahina kulizuka vurugu majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya kundi la watu wapatao 50 kuleta utata wakiwazuia kupiga kura wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Alliance kwa madai kuwa wanafunzi hao hawana sifa za kupiga kura.
Lakini mtendaji wa kata hiyo Ally Masatu ambaye ndiye alikuwa msimamizi msaidizi wa kituo hicho cha upigaji kura aliingilia kati na kutoa elimu kwa
wananchi hao kuhusu sifa za wanafunzi hao akiwataja kuwa ni wa kidato cha tano na cha sita na walijiandikisha baada ya kufikisha umri wa miaka 18.
* Huko wilayani Kwimba zoezi la upigaji kura lilichelewa kuanza kutokana na maeneo mbalimbali ya vijiji kucheleweshewa vifaa vya kupigia kura ambapo hadi majira ya saa 8:00
mchana hali ya upigaji kura ilikuwa bado.
Chapisha Maoni