mkoani Iringa HASSANI MTENGA, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa semtema mkoani Iringa.
Akiwahutubia mamia ya wananchi wa
mtaa wa semtema MTENGA aliwataka
wananchi wa eneo hilo kuwa makini wakati wa kuchagua kiongozi katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 14/12/2014.
MTENGA alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na watu binafsi kwa kuwa kila maendeleo yanaanzi chini ndio yanaenda juu,hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini sana na kumchagua kiongozi anayefaa.
aidha MTENGA aliwataka wanafunzi wa
vyuo vikuu mkoani iringa kuacha kuiga
siasa chafu ambazo waiga kutoka kwa
wapinzani wao kwa kuwa wanaiga kitu
ambacho hawakijua ambacho kitawaletea madhara baadae.
Alisema kuwa IRINGA ni ya watu wa iringa hivyo kuwaambia wanafunzi wa vyuo vyote mkoani iringa kuwaachia siasa wana iringa na wao waendelee na walicho kifuata hapa na sio isasa.
kwa upande wake wanafunzi
waliohudhuria mkutano huo walimsifu
katibu huyo wa chama cha mapinduzi kwa kuwa na sera zinazotekeleza na
kuwaambia ukweli vijana waliopo vyuoni
kwqa kuwa wananfunzi wengi wamekuwa wakiiga mambo mengi bila kujua nini kipo mbele yao.
lakini wananchi waliojitokeza eneo hilo
walimuita katibu huyo kwa jina dawa ya
muarobaini kwa maneno aliyoyatoa katika mkutano huo na kumsifu kiongozi huyo kuwa ni kiongozi ayefaa kuigwa hapa mkoani iringa.
pia kunabaadhi ya wananchi walisikika
wakisema kwa sera za katibu MTENGA
mbunge wa jimbo la iringa mjini atake
asitake ataondoka tu na kumwomba aanze kukusanya kilicho chake.
Chapisha Maoni