MWISHO wa safari. Liverpool imetupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia sare ya 1-1 nyumbani, Uwanja wa Anfield na FC Basle, hivyo kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye
Kundi B.
Fabian Frei aliifungia Basle bao la kuongoza dakika ya 25, kabla ya Lazar Markovic wa Liverpool aliyetokea benchi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60.
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard aliifungia timu yake bao la kusawazisha kwa mpira wa adhabu dakika ya 80 na haikuwa ajabu alipoibuka mchezaji bora usiku huu kwa timu yake, huku mchezaji bora wa mechi akiwa Luca
Zuffi wa Basle.
Mchezo mwingine wa Kundi B, vinara Real Madrid wamiechapa mabao 4-0 RFC Ludogorets Razgrad.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet,
Johnson, Lovren, Skrtel, Jose Enrique/Moreno dk45, Allen, Lucas/Coutinho dk74, Henderson na Gerrard.
Basle: Vaclik, Schar, Suchy, Safari, Elneny/Diaz dk83, Frei, Xhaka, Zuffi/Samuel dk88, Gashi, Gonzalez na Streller/Embolo dk74.
Chapisha Maoni