0
BAO la dakika ya 90+7 la beki Martin Skrtel limeinusuru Liverpool kulala nyumbani Uwanja wa Anfield baada ya kupata sare ya 2-2 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Beki huyo wa kati, Skrtel alifunga bao hilo muda mfupi tu baada ya Liverpool kumpoteza Fabio Borini aliyetolewa kwa kadi ya pili ya njano, akimalizia pasi ya Adam Lallana.

Philippe Coutinho alianza kuifungia Liverpool dakika ya 45 kwa pasi ya Jordan Henderson, kabla ya Mathieu Debuchy kuisawazishia Arsenal sekunde chache tu baadaye kabla ya
kipyenga cha mapumziko akimalizia pasi ya Mathieu Flamini.

Flamini alinusurika kutolewa kwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Adam Lallana, kabla ya Olivier Giroud kuifungia The Gunners bao la pili dakika ya 65.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Jones, Toure, Skrtel, Sakho, Lucas, Henderson, Markovic, Coutinho, Gerrard, Lallana na Sterling.

Arsenal; Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Chambers, Gibbs, Flamini, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Alexis, Giroud na Welbeck.

Chapisha Maoni

 
Top