
Wakuu wa Iraq wanasema mahujaji zaidi ya milioni 17 wamekusanyika Karbala kuhudhuria Arbaeen. Picha zilizopigwa kutoka angani zinaonesha barabara zinazoelekea Karbala kama mito ya watu
waliovaa nguo nyeusi, hadi upeo wa macho.
Na kuna wasiwasi kuwa mji wa Karbala hautaweza kuwapatia malazi waumini wote.
Ulinzi mkubwa umewekwa kuzuwia mashambulio ya wapiganaji wa Islamic State. Arbaeen ni siku ya mwisho ya maombolezi baada ya kifo cha Imam Hussain cha karne ya 7 katika vita vya Karbala - tukio muhimu ambapo Wasunni waligawanyika na Washia.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.