MABAO ya Samir Nasri na Pablo Zabaleta yameipeleka Manchester City katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji AS Roma
nchini Italia.
Mfaransa Nasri alifunga dakika ya
60, kabla ya Zabaleta kufunga la pili dakika ya 86, ushindi ambao unaihakikishia City kumaliza
katika nafasi ta pili kwenye Kundi E, nyuma ya Bayern Munich, ambao waliifunga CSKA Moscow 3-0 jana.
Ushindi wa Bayern dhidi ya CSKA unamaanisha City hata kama wangetoa sare wangefuzu City ambao jana waliwakosa nyota wao Sergio
Aguero, Vincent Kompany (wote majeruhi) na Yaya Toure anayetumikia adhabu, wana kila sababu ya kumshukuru kipa wao, Joe Hart kwa
kazi nzuri hadi Mchezaji Bora wa Mechi.
Kikosi cha Roma kilikuwa: De Sanctis, Maicon/ Florenzi dk79, Manolas, Yanga-Mbiwa, Holebas, Ljajic/Iturbe dk67, Nainggolan, Keita, Gervinho,
Pjanic na Totti/Destro dk70.
Man City: Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Clichy, Jesus Navas/Silva dk67, Fernandinho, Fernando, Milner, Nasri/Kolarov dk88 na Dzeko/Jovetic dk78.
Chapisha Maoni