BEKI wa Manchester United, Chris Smalling atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki mbili baada ya kuumia nyonga usiku wa Jumatatu akiichezea timu yake dhidi ya Southampton katika Ligi Kuu
ya England.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England ataikosa mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu dhidi ya mahasimu Liverpool Uwanja wa Old Trafford, na mechi itakayofuata dhidi ya Newcastle na labda pia atakosa mchezo wa Boxing Day nyumbani.
Smalling anaumia tena baada tu ya kurejea uwanjani kufuatia kuwa nje kwa muea mrefu kwa maumivu ya misuli, jambo ambalo linaanza kuleta shaka labda ni sababu ya mazoezi magumu ya kocha wa United, Mholanzi Louis
van Gaal
Mashetani hao Wekundu, tayari kwa sasa wanawakosa nyota wao wapya, Angel di Maria, Daley Blind na Luke Shaw, ambao wote ni majeruhi, wakati Rafael na Phil Jones ndiyo kwanza wanarudi uwanjani baada ya kupona..
Chapisha Maoni