0
CHELSEA imefuzu hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sporting Lisbon Uwanja wa Stamford Bridge usiku.

The Blues sasa inaungana na Schalke kufuzu hatua hiyo kutoka Kundi G baada ya timu zote kushinda jana.

Kocha Mreno, Jose Mourinho aliwapumzisha wachezaji wake kadhaa nyota, lakini Chelsea iling’ara kutokana na mabaoya Cesc Fabregas kwa penalti dakika ya nane baada ya Filipe Luis
kuchezewa rafu kwenye boksi, Andre Schurrle aliyefunga la pili dakika ya 16 na John Mikel Obi la tatu dakika ya 56.

Jonathan Silva ndiye aliyeifungi bao la kufutia machozi Sporting Lisbon dakika ya 50.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Cech, Azpilicueta, Zouma, Cahill, Filipe Luis, Mikel, Matic, Schurrle/Ramires dk74, Fabregas/Loftus-Cheek dk83, Salah/Remy dk71 na Diego Costa.

Sporting Lisbon; Rui Patricio, Ricardo Esgaio, Mauricio, Paulo Oliveira, Silva, Adrien Silva, William Carvalho/Montero, Jaoi Mario/Andre Martins, Carillo, Slimani, Capel/Carlos Mane
dk61.

Chapisha Maoni

 
Top