0
MSHAMBULIAJI Luis Suarez jana amefunga bao lake la kwanza Barcelona ikishinda 3-1 dhidi ya PSG katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Camp Nou, huku
Lionel Messi akiweka rekodi mpya Ulaya.

Barca iliyomaliza na pointi 15 na PSG pointi 13, zote zinafuzu hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya matokeo ya jana. 

Zlatan Ibrahimovic aliifungia bao la kuongoza PSG dakika ya 15, kabla ya Lionel Messi kuisawazishia Barca dakika nne baadaye akimalizia krosi ya Suarez.

Neymar akafunga bao la pili kwa Barca dakika ya 41, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Suarez kufunga la tatu dakika ya 77.Kwa Messi, sasa anafikisha mabao 76 kwenye michuano ya Ulaya na kuifikia rekodi ya gwiji wa Real Madrid, Raul katika ufungaji bora wa kihistoria wa michuano hiyo. Amefunga mabao
75 katika Ligi ya Mabingwa na moja katika Super Cup.

Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Bartra/Adriano dk92, Pique, Mathieu, Busquets, Mascherano, Iniesta/Xavi dk72, Pedro/Rakitic dk67, Messi, Luis Suarez na Neymar.


PSG: Sirigu, Van der Wiel, Thiago Silva, David Luiz, Maxwell, Verratti/Pastore dk62, Motta, Matuidi/Lavezzi, Lucas Moura, Ibrahimovic na
Cavani.

Chapisha Maoni

 
Top