Hali hiyo lisibabisha wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao walifurika kwenye kituo cha kupigia kura kilichopo
Mtaa huo, kupinga matokeo hayo kwa madai kuwa hawajapiga kura iweje matokeo Mwanza .
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakazi wa Mtaa wa Ibungilo B, Kata ya Ibungilo, Wilaya ya Ilemela mkoani hapa, wamekumbwa na hali ya
sintofahamu wakati wakijianda kupiga
kura ya kumchagua Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa huo, baada mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM kutangazwa
mshindi kabla ya wao kupiga kura.
Hali hiyo lisibabisha wafuasi wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) ambao walifurika kwenye
kituo cha kupigia kura kilichopo Mtaa
huo, kupinga matokeo hayo kwa madai
kuwa hawajapiga kura iweje matokeo
yatangazwe.
Hatua hiyo ilisababisha Polisi kuingilia
kati kuwatawanya wafuasi hao kwa
kupiga mabomu ya machozi, jambo
ambalo lilisababisha wafusi hao
kutawanyika sambamba na wananchi
waliyojitokeza kupiga kura.
Wakati hayo yakitokea Mbunge wa
Ilemela, Highnes Kiwia alimsimika
mgombea wa Chadema, Ramadhani Saidi kuwa Mwenyekiti wa Mtaaa huo, kwa madai kwamba ndiye chaguo la wakazi wa Mtaa huo na kwamba hawawezi kuchagulia kiongozi wasiyomtaka.
Kiwia alisema, “Haiwezekani watu
wamejitokeza kupiga kura, wanakuta
matokeo tayari yamebandikwa, ni jambo
la ajabu na lakushangaza watu
hawajapiga kura matokeo
yanapatikanaje, lazima suala hilo litolewe ufafanuzi wa kina.”
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi
alimtafuta msimamizi wa uchaguzi huo
Wilaya ya Ilemela ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi wilaya hiyo, Justin Lukaza,
na kueleza kwamba matokeo hayo ni
sahihi, kwani uchaguzi wa Disemba 14
walishindwa kutangaza matokeo
kutokana na tofauti zilizotokea, hivyo leo
wameamua kuyatoa.
Akizungumza na mwandishi wa gazeiti
hili Katibu wa Chadema tawi la Ibungilo
B, Abedi Bulashi alisema kuwa uchaguzi
ulifanyika Disemba 14, ulimalizika usiku
wa manane, lakini kulitokea kasoro na
msimamizi wa uchaguzi huo aliharisha
uchaguzi na kupanga kurudiwa leo
(jana).
Mmmo ya wananchi yao Daniel Buzuka
alisema, “Mimi nilifika asubuhi hapa
kituoni kupiga kura, lakini nilishangaa
kuona polisi wanakuja na kusema
hakuna uchaguzi, huu ni ubabe
umetumika na wametunyima haki yetu
ya masingi
MWANANCHI
Chapisha Maoni