0
Jeshi la Polisi mkoani Kagera limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wakiandamana huku wakifurahia ushindi walioupata katika uchaguzi wa serikali za
mitaa.

Akizungumza mara baada ya kuwatawanya wananchi hao Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe amesema jeshi hilo
lilipiga marufuku wananchi kuandamana bila kibali maalumu na kusabisha vurugu zisizo kuwa za lazima mitaani na akaongeza kuwa chama chochote kitakachofanya maandamano bila kibali
maalumu kitachukuliwa hatua za kisheria.

Nao baadhi ya wananchi ambao walikuwa katika maandamano hayo wamesema maandamano yao
yalikuwa ya amani na walikuwa wanafurahia ushindi walioupata katika uchaguzi huo na kwamba sasa wameamua kufanya mabadiliko kwa
kuwa wamechoshwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwakuwa imekuwa ikiwafumbia macho
viongozi wa chama hicho ambao wameshiriki katika wizi wa pesa za Escrow huku wananchi wakiendelea kubaki masikini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CHADEMA katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejey amesema sasa wakati umefika wakufanya mabadiliko na
wameibuka na ushindi katika mitaa 30 kati ya mitaa 66 iliyoko katika manispaa hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top