LICHA ya kucheza bila nyota wake kibao wa kikosi cha kwanza kama, Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, Gareth Bale na wengineo, RealbMadrid imetinga 32 Bora ya Kombe la Mfalme baada ya kuifumua Cornella mabao 5-0 usiku
Uwanja wa Bernabeu.
Cornella walipoteza penalti dakika ya 15, kabla ya James Rodriguez kuwafungia wenyeji bao la kwanza dakika ya 16 na Isco kufunga la pili dakika ya 32.
Mfungaji bora wa Kombe la Dunia aliye katika msimu wake wa kwanza Real, James akafunga tena bao la pili dakika ya 34, kabla ya bao la kujifunga la Borja Loez dakika ya 60.
Jese Rodriguez akahitimisha ushindi huo mnono ambao unakuwa wa 17 mfululizo kwa Real Madrid kwa bao la dakika ya 77. Real inasonga mbele kwa ushindi wa jumla mabao 9-1, baada ya awali kushinda 4-1 ugenini.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Pacheco, Arbeloa, Varane/Llorente dk46, Nacho, Coentrao, Illarramendi, Khedira/Jese dk57, Medran, James, Isco na Hernandez.
Cornella: Aberto, Pere, Borja, Pelegri, Israel, David, Luis, Gomez, Oscar Munoz/Trujillo dk56 na Gallar, Boniquet.
Chapisha Maoni