0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezoa viti vingi vya vitongoji, mitaa na vijiji vilivyokuwa vikikaliwa na Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wilayani Tarime.

Matokeo ya awali yanaonesha Chadema
imeshinda vitongoji zaidi ya 100 kati ya vitongoji 503, mitaa zaidi ya 30 na vijiji zaidi ya 30 kati ya vijiji 88.

Awali Chadema walikuwa na vijiji 4 na vitongoji zaidi 13. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Athuman Akalama na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime,
Venance Mwamengo walisema kuwa matokeo yasiyo rasmi ya awali, uchaguzi ulikwenda vizuri.

Lakini, walisema kulikuwepo na changamoto kadhaa, zikiwemo za kufariki kwa mwenyekiti wa Mtaa wa Gamasara, Wankyo Matiko na vurugu za
hapa na pale ambazo hazikuwa na madhara makubwa.

Chadema kimepata ushindi katika kata za Sirari, ambapo kimezoa viti vyote 4 vya vijiji na vitongoji 13. Chama Cha Mapinduzi kimepata viti viwili.

Katika kata ya Nyamaraga, Chadema kilipata viti vitatu na CCM kilipata kiti kimoja cha kijiji. Katika Kata ya Pemba, Chadema kilipata viti 3 vya kijiji na vitongoji 7 na NCCR Mageuzi kiti kimoja
kimoja cha kijiji. CCM haikupata kitu katika kata ya Mbogi, Chadema ilipata Vijiji vitatu.

Katika kata ya Kemambo, Chadema kilipata viti vya vijiji 3 na CCM kiti kimoja. Katika kata ya Nyarukoba, CCM ilipata viti 2 na Chadema
haikupata kitu.

Kata ya Matongo Chadema walipata viti 3 na CCM kiti kimoja. Kata ya Nyamwaga Chadema ilipata viti vyote 4 vya Kijiji. Katika kata ya Mriba,
Chadema viwli na CCM ilipata viti 2.

Katika kata ya Itiryo, Chadema ilipata viti vyote 3 vya Kijiji. Kata ya Nkende, CCM ilipata viti tisa na CCM ilipata viti 7. Katika kata ya Nyandoto, CCM
ilipata viti 6 na Chadema viti 4. Katika kata ya Bomani, CCM ilipata viti 5 Chadema viti viwili.

Chapisha Maoni

 
Top