0
Mamia ya wananchi na wafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA katika kata ya Kumsenga wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wameandamana kupinga wagombea wa UKAWA kuondolewa katika uchaguzi wa serikali za vijiji uliofanyika jumapili iliyopita katika vijiji vya kata
hiyo kutokana na hila za maafisa wa serikali.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilayani Kibondo mkoani Kigoma aliyengoza maandamano hayo Nicolaus
Kilunga, amesema UKAWA haikubaliani na wagombea wao kuengekuliwa na wananchi kuongozwa na viongozi wa CCM wasiowataka ambao wamepita bila kupingwa katika vijiji vya Kumsenga, Kukinama na Kibuye kwa madai ya
kutotimiza vigezo kwa wagombea wa upinzani na kwamba watadai haki hiyo mahakamani.

Kwa upande wao wananchi na wagombea walioengeliwa wamesema walifanyiwa hujuma na watendaji wa vijiji ambao hawakutoa fomu kwa
wakati na hawakuwepo ofisini na kwamba kutokana na hujuma hiyo hawako tayari kushirikiana na serikali zilizochaguliwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo isipokuwa
shughuli za msiba.

Chapisha Maoni

 
Top