0
Aliyekuwa waziri wa usalama Joseph Ole Lenku



Rais Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi waziri wa usalama Joseph Ole Lenku na kumpendekeza waziri mpya wa usalama Joseph Nkaiseri kuchukua
nafasi hio.

Wakati huohuo mkuu wa polisi nchini Kenya inspekta generali David Kimaiyo amejiuzulu kutokana na shinikizo dhidi yake afanye hivyo kwa kushindwa kukabiliana na utovu wa usalama
nchini.

Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya
mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali 'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
Rais alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.

Aliyekuwa mkuu wa polisi David Kimaiyo
Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake.

Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa
utovu wa usalama nchini. Hatua ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao
wawili hao bila shaka litakuwa jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini.

Uteuzi wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya
serikali.

Alipokuwa anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza mda wa vikao vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa
kuchukua nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili wamuidhinishe.




chanzo BBC

Chapisha Maoni

 
Top