KOCHA wa Ujerumani, Joachim Low ametajwa kuwa kocha Bora wa Mwaka wa Dunia katika sherehe za FIFA utoaji tuzo za Mwanasoka Bora wa Dunia zinazoendelea mjini Zurich, Uswisi.
Low amewapiku makocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti na Atletico, Diego Simeone kushinda tuzo hiyo baada ya kuiongoza Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia nchini Brazil kwa mara ya nne mwaka jana.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 54 aliisaidia Ujerumani kumaliza ukame wa miaka 18 wa kusubiri taji hilo kwa kuifungaArgentina katika Fainali, bao pekee la Mario Gotze dakika
za nyongeza.
Chapisha Maoni