Maandamano ya umoja nchini Ufaransa yaanza Maandamano ya umoja nchini Ufaransa yameanza baada ya makundi ya watu kukongamana katika eneo la de la Republique katika mji mkuu wa
Paris nchini Ufaransa ,kama kigezo cha
kuonyesha umoja dhidi ya mashambulizi ya wiki iliopita yaliotekelezwa na waislamu wenye itikadi kali.
Zaidi ya watu millioni moja wanashiriki katika maandamano hayo.
Makumi ya viongozi wa nchi tofauti duniani wako mji paris ambapo usalama umeimarishwa huku maafisa zaidi wa jeshi na wale wa polisi wakiwekwa kupiga doria.
Ghasia hizo nchini Ufaransa zilianza siku ya jumatano kutokana na shambulizi la gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Hatahivyo maafisa wa polisi waliwazingira na kuwapiga risasi mandugu wawili waliohusika na
shambulizi hilo.
Chapisha Maoni