
Tukio hilo limevuta mamia ya wananchi
ambao wamefika katika hospitali ya rufaa mkoa wa mara mjini musoma kwa lengo la kutaka kushuhudia tukio hilo.
Akizungumza na Mpekuzi katika wodi ya
wazazi katika hospitali hiyo ya rufaa ya
mkoa wa Mara mjini Musoma, muuguzi wa zamu Bi Naabu Geraruma, amesema kuwa mwanamke huyo amefanikwa kujifungua usiku wa saa Saba kwa njia ya Operesheni watoto hao wawili wenye jinsi ya kike huku wakiwa na uzito wa kilo 4.6.
Hata hivyo muuguzi huyo wa zamu amesema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika hospitali ya mkoa wa Mara na kwamba hali za mwanamke huyo na watoto zinaendelea
vema na taratibu za kumpeleka hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza zimekamika.
Taarifa ambazo zimeifikia Mpekuzi baadaye kutoka jijini Mwanza na kuthibitishwa na mkurugenzi wa utawala na rasmali watu wa hospitali ya rufaa ya Bugando Bi Leah Kagine zinasema tayari mwanamke huyo na watoto wamefikishwa katika hospitali ya rufaa
kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
Picha za watoto waliozaliwa wameungana
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.