0
Afande Sele amedai kuwa Daz Baba
havuti unga kama watu wengi
wanavyodhani bali amekuwa akinywa
pombe bila kuzingatia kula hali
inayomfanya akonde.

Akiongea na paparazi, Afande amesema
huu ni wakati wa wasanii na wadau wa
muziki nchini kuonyesha juhudi za
kumuokoa katika hali hiyo ili kunusuru
maisha yake.

“Tatizo sisi wabongo tunapenda kusema
vitu vya unafiki hasa hasa sisi wasanii,”
amesema Afande. “Tunashindwa kusema vitu vya ukweli mwisho wake
tunaathirika zaidi.

Mbona wasanii wengine wa nje
wakifilisika wanasema wamefilisika ili
waweze kuishi maisha ya kawaida?”
amehoji Afande.

“Tatizo watu wanajikweza wakati
hawana kitu. Kusema kweli hali halisi ya
Daz Baba ni mtu ambaye kama
kachanganikiwa hivi.

Daz Baba havuti unga. Wasanii acheni
kuongea huu ndio wakati wa kumsaidia.
Daz Baba akinywa pombe hata bia mbili
tu anabadilika kabisa na tatizo lake Daz
akinywa pombe hawezi kula, kwahiyo
mara nyingi anakesha anakunywa
pombe, hachagui pombe. Kusema kweli
Daz Baba ni mtu ambaye kachakaa.

Mimi naapa Daz havuti unga ila ni mlevi
kupita kiasi. Hana muda wa kulala.
Ukikutana naye sehemu unamwomba
msamaha wewe kwa sababu bila hivyo
atakusumbua na haelewi anachoongea,
kama vile chizi tu.

Wapo wadau ambao wanajua Daz katoka wapi. Mimi mwenyewe binafsi
nimeshahangaika na Daz na kwa namna
ya pekee lakini watu wengine hawafikirii
kama hili jambo ni la serious.”
“Toka naanza kubadilika mimi najaribu
kumweka sawa. Kwasababu kama hali
ngumu hata sisi hali ngumu tunahangaika tu.

Watu wengi wanasubiria mtu amekufa
halafu waanze kutoa magari na
michango. Kwanini kama mnaweza
kufanya juhudi hizo msifanye sasa hivi?
Kwenye mazishi watu wanajifanya
kukodi magari kwenda kuzika, mtu kama
Daz kipindi hiki ndio cha kumsaidia.

Wapo marafiki wa Daz, wasanii wadau
wanaweza kumsaidia sasa hivi.”

Chapisha Maoni

 
Top