PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima jana aliiomba mahakama kuahirisha tarehe yakusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu
anaumwa.
Kibatala alidai mahakamani Kisutu kuwa
kutotokea kwa mteja wake jana kulitokana na
yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Wakili huyo aliwasilisha madai hayo jana katika
Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya
Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi
anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima
Mahakama ilikubali ombi hilo na kwamba kesi
hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.
Katika kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha
ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo
la Dar es Salaam.
Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16
na 25 Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya
Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es
Salaam.
Mpekuzi blog
Chapisha Maoni