0

Yanga imefanikiwa kumaliza utata wa kuendelea na
kocha wao mkuu Hans Pluijm baada ya
kumuongezea mkataba wa miaka miwili.
Mkataba wa Pluijm na Yanga ulifikia tamati mwezi
mmoja uliopita ambao ndiyo umeipa klabu hiyo
mafanikio ya kutwaa taji la ubingwa wa Ligi kuu
Tanzania Bara mara mbili, Kombe la FA pamoja na
kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
Kocha Pluijm amesema anafuraha ya kuendelea
kuifundisha Yanga ambapo sasa anataka
kuhakikisha anaendeleza kazi na mafanikio zaidi
kwa Yanga kuweza kufika mbali katika mashindano
ya CAF mwakani.
Pluijm amesema, anaipenda Yanga na sikuzote
amekuwa akifanya kazi kwa kutanguliza heshima.
Pluijm amesema, changamoto yake kubwa kwa
sasa ni kuhakikisha Yanga inafanya vizuri zaidi
japo haitakuwa kazi rahisi.
Mkataba huo wa Pluijm ambaye wikiendi iliyopita
aliibuka kuwa kocha bora wa msimu uliopita
ameusaini mbele ya katibu mkuu wa Yanga Baraka
Deusdedit.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top