0
MSHAMBULIAJI Zlatan
Ibrahi  Mshambuliaji huyo wa
Sweden anatarajiwa
kufanyiwa vipimo vya afya
Ijumaa baada ya kufikia
makubaliano ya Mkataba na
United wiki kadhaa zilizopita
kwamba atalipwa Pauni
200,000 kwa wiki.
Ibrahimovic ameposti picha
ya nembo ya Manchester
United akiambatanisha na
maelezo yasemano: "Wakati
wa kuifahamisha dunia,".
Alimalizia katika maelezo
yake chini ya picha kwa
kuandika '#ninakuja'.
Nyota huyo wa zamani wa
Barcelona na Inter Milan,
alikataa kuongeza Mkataba
katika klabu yake, Paris
Saint-Germain na mapema
ilifahamika atakwenda
kuungana na Mourinho
aliyechukua nafasi ya Louis
van Gaal Uwanja wa Old
Trafford.
Atasaini rasmi Mkataba
Ijumaa na kuwa mchezaji wa
pili kusajiliwa na Mourinho’
tangu atambulishwe kuwa
kocha mpya wa United.
Mourinho wakati wote
alipenda kuungana tena na
Ibrahimovic aliyewahi kufanya
naye kazi kwa mafanikio
walipokuwa Inter Milan ya
Italia.
Baada ya kumalizana na
Ibrahimovic, United imeingia
rasmi kwenye majadiliano na
Juventus ya Italia juu ya
kiungo kumsajili tena kiungo
wake wa zamani, Mfaransa
Paul Pogba.
Kwa mujibu wa gazeti la
L'Equipe la Ufaransa, Pogba,
mwenye umri wa miaka 23
sasa, aliyeondoka Man United
kuhamia Juventus kama
mchezaji huru mwaka 2012
baada ya kukataa kuongeza
Mkataba chini ya kocha Sir
Alex Ferguson kutokana na
kutopewa nafasi ya kucheza,
sasa anaweza kurejea Old
Trafford.
Chini ya Ferguson, Pogba
alicheza mechi saba tu za
kikosi cha kwanza Man
United, lakini sasa chini ya
kocha Mreno, Jose Mourinho
Mashetano hao Wekundu
wanataka kumrejesha Old
Trafford.
Na inasemekana Juve,
maarufu kama Kibibi Kizee
cha Turin haiwezi kumuuza
nyota wake huyo kwa dau la
chini ya Pauni Milioni 82.8..
L'Equipe limesema kwamba ,
kocha mpya wa Man United,
Jose Mourinho anataka
kutambulisha mfumo wa
4-3-3 msimu ujao na
anamtaka Pogba akachezea
pamoja na Nahodha Wayne
Rooney katika safu ya kiungo
katikati, pamoja na
mshambuliaji Zlatan
Ibrahimovic, Anthony Martial
na Henrikh Mkhitaryan
pembeni.vic hatimaye
amethibitisha anakwedna
Manchester United msimu
ujao.
Mkongwe huyo mwenye umri
wa miaka 34 safari yake ya
kwenda kuungana na kocha
Jose Mourinho imekuwa
moja ya siri zilizotunzwa
vizuri katika soka.
Hata hivyo, Ibrahimovic
ameamua kuthibitisha hilo
Alhamisi kupitia ukurasa
wake wa Instagram soka
moja nyuma kabla ya
ilivyotarajiwa.
Zlatan bado hajasaini
Mkataba Man United wala
kufanyiwa vipimo vya afya,
lakini wamefurahia mchezaji
huyo kutangaza habari hizo.  

Chapisha Maoni

 
Top