0
TIMU za Wydad Casablanca
ya Morocco na Mamelodi
Sundowns zinaongoza
maakundi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika baada ya
mechi za katikati ya wiki hii.
Wydad
Casablanca iliifunga 2-0 Zesco
United juzi mjini Casablanca
na kufikisha pointi sita katika
Kundi A, mbele ya ASEC
Mimosa iliyoshinda 2-1
ugenini dhidi ya Al Ahly mjini
Cairo Misri na kupata pointi
tatu za kwanza, wakati Zesco
pia ina pointi tatu na Al Ahly
haina pointi inashika mkia.
Mamelodi Sundowns
ilishinda 2-1 nyumbani dhidi
ya Enyimba ya Nigeria
Jumanne na kupata pointi
tatu za kwanza hivyo
kuongoza Kundi B kwa
wastani wa mabao, ikilingana
pointi na Zamalek ya Misri
ambayo haikuwa na mechi
baada ya CAF kuiondoa ES
Setif ya Algeria mashindanoni
kwa vurugu za mashabiki
wake.
Enyimba inashika mkia katika
kundi hilo ikiwa haina pointi
baada ya kucheza mechi,
tofauti na wapinzani wake,
Mamelodi na Zamalek
ambazo kila moja imecheza
mechi moja.
ES Setif iliondolewa kufuatia
vurugu kubwa zilizofanywa
na mashabiki wake katika
mchezo dhidi ya Mamelodi
Sundowns ya Afrika Kusini
Juni 19 iliyopita.
Ripoti ya marefa ilisema
amani ilichafuka uwanjani
baada ya mashabiki kurusha
mioto, chupa na mawe na
kusababisha watu kadhaa
kujeruhiwa kabla ya walinzi
kuingilia kati kutuliza hali
hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top