Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema watu
wanaweza kushangazwa na Simba kuwaacha
washambuliaji wake wanaong’ara kwenye Ligi Kuu
Bara lakini kumekuwa na sababu tofauti huku
akisema Hamisi Kiiza, alikuwa tatizo na
mtengeneza matatizo ndani ya kikosi cha Simba.
Manara amemtaja Kiiza kama chanzo cha
matatizo, asiye mvumilivu na mbinafsi kupita
wachezaji wote waliowahi kuichezea Simba.
“Kiiza kweli alifunga mabao 19 kwenye ligi, lakini
kwa aina ya uchezaji wa Simba angefunga hata
zaidi ya 25. Lakini tabia yake ni mtu muanzisha
matatizo, ni tatizo kubwa kuliko unavyofikiri.
“Kila mara alikuwa anaanzisha migogoro,
mshahara ukichelewa siku tatu anaanza kulaumu.
Mfano kuna siku nilikwenda mazoezini kwa niaba
ya uongozi kuwaeleza wachezaji kuwa mshahara
tayari umeingizwa benki.
“Nikawasubiri wamemaliza mazoezi, wakaambiwa
ninataka kuzungumza naye. Wakati naanza tu
kuzungumza, yeye akarukia na kuanza kusema
mishahara leo ni tarehe tatu, anasikitika sana.
Nikamuuliza unajua kilichonileta hapa? Vipi
hausikilizi hata kiongozi anachoongea halafu nawe
useme yako.
“Ni mtu asiye na subira, tukifika hotelini anataka
chumba chake kiwe tofauti na wengine. Anataka
achelewe kuja kula, lakini awekewe. Anataka
kwenye basi achelewe, limsubiri. Kwa kifupi ni mtu
anayeua morali ya wachezaji kwa kiwango cha juu
kabisa.
“Nikuhakikishie kama Kiiza angebaki msimu huu,
mimi ningeondoka. Maana kungekuwa hakuna haja
ya kupambana halafu ndani ya timu kuna ‘kirusi’
kinawatafuna,” alisema Manara.
"Kuhusiana na Amissi Tambwe, ukweli ule ulikuwa
ni mfumo wa mwalimu Phiri, ilionekana haendani
na mfumo naye akaamua aondoke.
"Alikuwa akimuweka benchi na akiingia hafanyi
vizuri hata katika mechi za kirafiki. Uongozi
ulimuamini kocha ndiyo maana ukatekeleza
alichosema," alisisitiza Manara.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports 👉👉 https://m.facebook.com/JohnNgassaBlogspot/?ref_component=mbasic_bookmark&ref_page=XMenuController Posted: ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni