Kikosi cha Simba kilichosukwa upya na kocha
Joseph Omog kimelazimishwa sare ya bao 1-1 na
timu ya URA katika mchezo wa kirafiki uliopigwa
kwenye dimba la Taifa.
Mchezo huo ulikuwa maalum kumuaga aliyekuwa
mshambuliaji wake mkongwe, Mussa Hassan
'Mgosi' aliyetangaza kustaafu mwanzoni mwa wiki.
Simba ilikuwa ya kwanza kufungwa kwenye dakika
ya 20 lakini ilifanikiwa kurudisha kupitia kwa
nahodha wake Jonas Mkude.
Mgosi ameteuliwa kuwa Meneja wa klabu ya
Simba hivyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo
licha ya kustaafu leo.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni