Jose Mourinho, mkufunzi wa Manchester United
ameanza kwa furaha msimu mpya wa ligi kuu ya
Uingereza baada ya timu yake kupata ushindi wa
mabao 3-1 ugenini dhidi ya Bournermouth.
Huo ni ushindi muhimu kwa kocha huyo msema
hovyo aliyejipambanua kutaka kutwaa kila taji
msimu huu.
Bournermouth ilicheza vyema dakika 35 za kipindi
cha kwanza kabla Simon Francis hajafanya makosa
ya kizembe kwa kumrudishia kipa wake mpira
mfupi ulioishia miguuni mwa Juan Mata ambaye
alifunga kwenye jaribio la pili baada ya mpira
aliopiga awali kuokolewa na golikipa kisha
kumgonga Francis kwa mara ya pili na kumrudia
Mata.
Kipindi cha pili Manchester United iliimarika zaidi
na kufanikiwa kufunga mabao mawili zaidi kupitia
kwa Wayne Rooney na Zalatan Ibarahimovic,
mchezaji anayetabiriwa kuipa mafanikio makubwa
Man Utd msimu huu.
Ibrahimovic amefunga bao lake la tatu tangu
ajiunge Man Utd, bao moja akifunga kwenye
mchezo wa kirafiki na jingine alilifunga wiki
iliyopita wakati Man Utd ilipoibuka na ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Leicester katika mchezo wa
ngao ya jamii.
Bao la kufutia machozi kwa upande wa
Bournermouth lilifungwa na Adam Smith.
Ushindi huo unaifanya Man United ikae kileleni
kwenye msimamo wa ligi kwa michezo iliyopigwa
mpaka sasa.
Erick Baily ameonyesha kuwa nguzo muhimu kwa
Manchester United upande wa ulinzi, kwa mchezo
wa leo yeye ndio anastahili kuwa nyota wa mchezo
huo kutokana na utulivu na uimara aliyo onyesha.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni