TP Mazembe imekubali kipigo cha mabao 3-2 ikiwa ugenini dhidi ya Medeama katika
mechi ya Kombe la Shirikisho, leo.
Ushindi huo wa Medeama, maana yake imefikisha pointi 8 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga huku Mazembe ikiwa
kileleni na pointi 10.
Baada ya ushindi wa Medeama, maana yake rasmi Yanga ambayo jana iliifunga Mo
Bejaia imeshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali licha ya kuwa na mchezo mkononi.
Yanga inabaki na pointi nne mkiani, huku
Mo Bejaia ikilazimika kutupa karata yake ya
mwisho kwa kutaka kuifunga Medeama
katika mechi ya mwisho ili ifikishe pointi
nane huku ikijaribu kuangalia wastani wa
mabao ya kufunga na kufungwa.
Yanga itamaliza mechi yake ya mwisho
dhidi ya TP Mazembe ikiwa ugenini mjini
Lubumbashi.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni