Manara amethibitisha kuwa mechi ya kirafiki
Simba dhidi ya URA itakuwa maalumu kwa
kumuaga Mgosi anayestaafu soka, fuatilia
matukio yote Goal
Mchezaji mkongwe wa Simba SC Musa Hassan
Mgosi Jumapili ya 14 Agosti 2016 ataagwa rasmi
kama mchezaji wa klabu hiyo atakapokuwa
akistaafu rasmi kucheza soka la ushindani.
Mgosi ataagwa kwenye mchezo wa kirafiki kati ya
Simba dhidi ya URA ya Uganda utakaochezwa
kwenye uwanja wa taifa.
Kuelekea mchezo huo, afisa habari wa Simba SC
Haji Manara amethibisha kwamba Mgosi atalipa
soka kisogo na amepewa nafasi ya kuwa meneja
wa klabu hiyo mara baada ya kutangaza
kustaafu.
“Licha ya kwamba mechi dhidi ya URA itawapa
fursa benchi la ufundi kuangalia na kufanya
masahihisho ya mwisho kabla ya ligi kuu kuanza
wiki ijayo, tutatumia mechi hiyo pia kumuaga
mchezaji wetu Musa Hassan Mgosi ambaye tayari
anastaafu rasmi kucheza soka la ushindani,”
amesema Manara.
Haji amesema Mgosi atacheza, mechi hiyo kwa
dakika chache kisha baadaye atastaafu kwa
kushika mpira na kuubusu na kufanya mambo
mengine ambayo hufanywa wakati mchezaji
anapotangaza kustaafu kisha kuwapungia mkono
mashabiki.
Msemaji huyo wa Wekundu wa Msimbazi
aliendelea kusema kwamba, baada ya zoezi la
kustaafu, Mgosi ataingia kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo ambapo atabadili nguo na
kurudi uwanjani akiwa kama maneja .
“Baada ya Mgosi kustaafu anakuwa meneja mpya
wa Simba wakati Abasi Ali ataendelea kuwa
mratibu, kwa pamoja watu hawa wawili watakuwa
wanashirikiana huku mmoja akiwa karibu zaidi na
benchi la ushindi kwa maana ya Mgosi na
mwengine akifanya shughuli za kawaida za timu
nje ya benchi la ufundi lakini kwa ushirikiano wa
ndani.”
“Tunafanya hivi kwa ajili ya kuwapa motisha
wachezaji vijana kwamba unapocheza klabu ya
Simba kwa juhudi, nidhamu na mafanikio
unaendelea kuwa sehemu ya Simba. Kwahiyo
tunampa nafasi hiyo Mgosi tunajua ni mchezaji
aliyejituma sana, mwenye nidhamu kubwa na
uzoefu wa kutosha atashirikiana na uongozi
kuhakikisha msimu huu tunafanya vizuri.”
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni