Kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs
Dele Alli, amebadilisha jina litakalotumika kwenye
jezi yake mgongoni msimu huu kwasababu haoni
uhusiano wa moja kwa moja na jina la Alli na
sasa atakuwa akitumia jina na Dele kuanzia
msimu huu.
Awali Dele Alli alikuwa akitumia jina la Alli
mgongoni mwa jezi yake msimu uliopita vilevile
kwenye michuano ya Euro 2016.
Alli, 20, amesema: “Nataka niweke jina kwenye
jezi yangu ambalo lina uhusuiano wa moja kwa
moja na mimi, jina ambalo linaniwakilisha mimi
kama nilivyo na nahisi jina la Alli halina uhusiano
wa moja kwa moja na mimi.
“Huu sio uamuzi ambao nimekurupuka tu kufanya
bali ni uamuzi ambao umeridhiwa na familia
nzima kwa ujumla.”
Sababu kubwa za maamuzi hayo inaelezwa
kwamba, baba yake Dele Ali ambaye alikuwa
akiitwa Kenny Alli mwenye asili ya Kinigeria,
hakuhusika katika malezi ya mwanaye na hivyo
kupata shida katika makuzi yake kutokana na
mama yake kuwa mlevi kupindukia.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni