0

Klabu ya KRC Genk anayoitumikia Mtanzania
Mbwana Samatta, Jumamosi August 13
imeshindwa kutamba mbele ya Waasland
Beveren baada ya kubanwa na kulazimishwa sare
ya kufungana magoli 2-2 kwenye mchezo wa ligi
ya Ubelgiji.
Genk walitoka nyuma kwa magoli 2-0 hadi
kusawazisha magoli yote na kuambulia pointi
moja katika mchezo huo. Nikolaos
Karelis aliifungia Genk goli la kwanza dakika ya
35 kabla ya mchezaji wa Waasland Beveren
Laurent Jans kujifunga na hatimaye
kuisawazishia Genk. Magoli ya Waasland Beveren
yalikwamishwa kambani na Ibrahima
Seck aliyefunga dakika ya 6 na Jonathan
Buatu ambaye alifunga bao la pili.
Katika mchezo huo Samatta aliingia dakika ya 47
kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kebano.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya tatu katika ligi ya Ubelgiji
(Belgian Jupilier Pro League) ambapo hadi sasa
Genk inakamata nafasi ya 6 ikiwa na pointi tatu
baada ya kucheza mechi tatu ikifanikiwa kushinda
mechi moja, sare moja huku ikipoteza mchezo
mmoja.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top