Himid anakwenda kwenye klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo ligi inayojulikana kwa jina la Superliga Kiungo wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Himid Mao ameondoka nchini Mei 1, 2017
kuelekea Denmark kwa ajili ya majaribio ya kutafuta kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Himid anakwenda kwenye klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo ligi inayojulikana kwa jina la Superliga.
Kiungo huyo ameonesha kiwango cha juu katika msimu huu kuanzia kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara, kombe la Azam Sports Federation Cup, michuano ya kimataifa pamoja na mechi za timu ya taifa.
Kwa mujibu wa Shaffihdauda, Himid alisema kably ya kuondoka: “Naenda kwenye klabu ya Rander FC ya nchini Denmark kwa ajili ya majaribio kwa
muda wa siku 15, kama mchezaji najiamini naweza kufanya lolote sehemu yoyote, mambo mengine ya mbele anajua Mungu,” amesema
Himid muda mfupi kabla ya kuondoka ardhi ya Bongo.
“Mimi wajibu wangu ni kujitolea kadiri niwezavyn na kuwashawishi hao kwa uwezo wangu wote patakapobakia ni kazi ya Mungu.”
“Kila kitu kipo kama kilivyopangwa, klabu yangu inajua, wakala anajua kwa hiyo kila kitu kipo wazi utakapofika wakati wa klabu kutangaza chochote
watafanya hivyo.” “Kwa sasa naangalia hiki kilichopo mbele halafu
baadae tutajua nini kitakachofuata.”
Chapisha Maoni