Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid Christiano Ronaldo amekuwa mwiba mchungu
baada ya kuiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa hapo jana jumanne katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Ronaldo alipachika mabao hayo katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza na kuandika bao la pili
dakika ya 73 kipindi cha pili ,huku akihitimisha karamu ya mabao matatu dakika ya 86 kipindi cha
pili.
Na hii leo jumatano usiku inatarajiwa kupigwa nusu fainali nyingine kati ya Fc Monaco dhidi ya
Juventus huko Stade Louis jijini Monaco.
Na wakati huo huo Mshambuliaji nyota wa Fc Monaco Radamel Falcao amesema hana mpango
wowote wa kuondoka katika klabu hiyo ambayo inafukuzia mataji mawili msimu huu, la Ligue 1 na
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Real Madrid: Navas, Carvajal (Nacho 46 mins), Ramos, Varane, Marcelo, Kroos, Casemiro, Modric, Isco (Asensio 67), Benzema (Lucas 77), Ronaldo
Subs not used: Casilla, Rodriguez, Kovacic,Morata
Goal: Ronaldo 10, 73, 85
Booked: Isco
Atletico Madrid: Oblak, Lucas, Savic, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Saul (Gaitan 58), Carrasco (Correa 67), Griezmann, Gameiro
(Torres 57)
Subs not used: Miguel Moya, Tiago,
Thomas, Rodriguez
Booked: Koke, Saul, Savic
Referee: Martin Atkinson (England)
Chapisha Maoni