MSHAMBULIAJI wa zamani wa Real Madrid na Chelsea, Nicolas Anelka ametangaza kujiunga na Mumbai City ya Ligi Kuu ya India.
Imeripotiwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye amekuwa hana timu tangu aondoke West Brom Machi mwaka huu, amekubali mkataba wa muda
mfupi na timu ya ISL inayofundishwa na
Peter Reid.
"Ninayo furaha kujiunga na Mumbai City FC na nimevutiwa sana kujiunga na Ligi Kuu ya India," ameandika Anelka kwenye akaunti yake ya Twitter.
Chapisha Maoni