0
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro 'Chid Benz' amekamatwa na madawa ya kulevya aina ya heroine na bangi akiwa kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, jana.

Akizungumza Kamanda wa Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP, Alfred Nzowa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa msanii huyo alikuwa njiani kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

Kamanda Nzowa amesema kuwa Chid amekutwa na madawa hayo baada ya upekuzi wa kawaida uliokuwa ukiendelea uwanjani hapo, ambapo jeshi
la polisi linamshikilia kwa mahojiano na
uchunguzi zaidi.
“Ni kweli tumemkamata Rashid Makwiro maarufu kwa jina la Chid Benz akiwa na kete kumi na nne za madawa ya kulevya aina ya heroine pamoja na misokoto miwili ya bangi.
“Msanii huyo alikuwa njiani kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki, na sasa amewekwa katika sehemu maalum ambayo
hatuwezi kusema ni wapi, kwa sababu za kiusalama, uchunguzi wa tukio unaendelea.” Amesema kamanda Nzowa.
Taarifa zilizokuwepo awali zilisema kuwa Chid alikuwa njiani kwenda Mbeya kwa ajili ya kushiriki kwenye shoo ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika leo Jumamosi.
Chid ni kiongozi wa kundi la muziki la la Famila lenye makao makuu Ilala jijini Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

 
Top