Vipimo vya mgonjwa aliyetoka nchini Senegal na kuwekwa kwenye karantini mjini Moshi kwa tahadhari ya ebola, baada ya kukaa nchini kwasiku 14 vimepelekwa katika maabara ya jijini Nairobi nchini Kenya kwa uchunguzi.
Mbali na vipimo hivyo, lakini madaktari na wauguzi wote waliomhudumia na wanaendelea kumhudumia mgonjwa huyo, nao wamewekwa kwenye karantini wakisubiri majibu ya vipimo
hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Mtumwa Mwako wakati uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro ulipokutana na
wanahabari kutoa taarifa ya maendeleo na uchunguzi wa awali.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama mbali na kuwatoa hofu wananchi wa mkoa huo, lakini alisema maeneo yote
aliyopita mgonjwa huyo tangu aingie nchini wameyabaini na kuchukua tahadhari.
“Kwa kweli nampongeza sana mgonjwa
mwenyewe ametoa ushirikiano mkubwa sana. Hata magari aliyopanda akiwa hapa nchini rekodi zake tumechukua ili kama ikitokea majibu yakaja
tofauti tujue la kufanya,” alisema.
Chapisha Maoni