MABAO mawili ya Papiss Cisse yameipa ushindi wa 2-1 Newcastle dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya England, Chelsea katika mchezo uliofanyika Uwanja wa St James' Park jioni hii.
Katika mchezo huo ambao Steven Taylor
alitolewa nje zikiwa zimebaki dakika 10 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, kipigo hicho kinakuwa cha kwanza kwa timu ya Jose
Mourinho katika Ligi Kuu msimu huu.
Cisse alifunga bao la kwanza dakika ya 57 na la pili dakika ya 78 kabla ya mkongwe Didier Drogba kuifungia Chelsea bao la kufutia machozi dakika ya 83.
Chapisha Maoni