0
ARSENAL imechapwa mabao 3-2 ugenini na Stoke City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.

Mabao ya Peter Crouch dakika ya kwanza, Bojan Krkic dakika ya 35 na Jonathan Walters dakika ya 45, yaliifanya Stoke iongoze 3-0 hadi
mapumziko, kabla ya Gunners kuanza
kupambana kurudisha.

Crouch ameweka rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi katika Ligi Kuu ya England, kwani ilimchukua sekunde 19 tu kumuinamisha Arsene Wenger.

Arsenal ilipata mabao yake kupitia kwa Santi Cazorla kwa penalti dakika ya 68 na Aaron Ramsey dakika ya 70.
Calum Chambers alionyeshwa kadi nyekundu ya kwanza nyekundu tangu aanze soka baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 78.

Kikosi cha Stoke City kilikuwa; Begovic,
Bardsley, Shawcross, Muniesa/Whelan dk63, Pieters, Nzonzi, Cameron, Diouf/Adam dk69, Bojan/Huth dk86, Walters na Crouch.

Arsenal; Martinez, Bellerin/Welbeck dk46, Chambers, Mertesacker, Gibbs/Campbell dk90, Flamini, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Sanchez, Cazorla, Giroud/Podolski dk63.

Chapisha Maoni

 
Top