0
Zipo nyingi sana, lakini hapa nitakupa dalili ambazo ukiona mwanamke wako anazo ujue hana penzi la moyoni.

ANAKUTEKA
Mwanamke ana haki ya kudeka kwa
mwanaume wake, lakini siyo kwa nia
nyingine yoyote zaidi ya kunakshi penzi.
Huyu hana nia hiyo, anadeka kwa ajili ya
kukupagawisha kimahaba ili aweze
kuzishika hisia zako sawasawa.
Mchunguze vizuri, utagundua kwamba
hata sauti yake anayoitumia kuzungumza
na wewe siyo anayotumia akiwa na
shoga zake. Anailegeza kwa kuiremba
kwa kila hali.
Anataka kukupagawisha. Hiyo ndiyo nia
yake, kukupagawisha sana maana yake
hutapindua na hutakuwa na wazo la
kuwa na mtu mwingine zaidi yake.

ANAPENDA FEDHA
Ni kawaida mwanamke kumuomba fedha mpenzi wake, lakini huyu asiye na
mapenzi ya kweli, huwaza fedha mara
zote.
Hata kama utazungumza kuhusu kutoka
naye katika matembezi, bado ataulizia
kuhusu dau lake.
Ana mahitaji mengi. Mwanamke wa aina
hii, ukitoka naye nje ya mji au kulala
naye hotelini, asubuhi atataka chake!
Jiulize ni mpenzi wako au anajiuza?
Mbaya zaidi, hata kama utakuwa
mgonjwa na amekuja kukutazama siyo
ajabu kabisa kukuomba fedha, akiwa na
tabia hii ujue hana mapenzi, anataka
kukutumia.

HANA HESHIMA
Kwa kuwa hakupendi na wala hafikirii
kuwa na wewe katika ndoa, sifa za
uanamke hatakuwa nazo. Inawezekana
kabisa anazifahamu vizuri sana sifa hizo, lakini hana muda nazo.

Hasikii ukimwambia kitu, mjeuri na wala
haheshimu kauli zako.
Kama mpenzi wako, ambaye una
malengo naye ya baadaye, una haki ya
kumzuia aina fulani ya mavazi, kampani
au tabia ambazo huzipendi.
Kwa mwanamke wa aina hii,
kumwambia ni sawa na kumruhusu!
Mwanamke huyu, neno heshima ni
msamiati mgumu sana kwake.
Unajua kwa nini? Kwa sababu hakupendi

Chapisha Maoni

 
Top