0
WATANI wa Jadi Simba na Yanga
wanaendelea kuvutana vikali katika dhindano la 'Nani Mtani Jembe2' linalodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa timu hizo zenye upinzani mkubwa hapa nchini.

Shindano hilo lililoanza kutimua vumbi
mwanzoni mwa mwezi huu na kutarajiwa kufikia tamati Disemba 13 mwaka huu kwa kumenyana katika uwanja wa Taifa linazidi kushamili zaidi kutokana na upinzani wa kuvutana baina ya mashabiki wa pande hizo.

Kwa mujibu wa Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe kampeini hiyo imeonekana kupendwa na mashabiki wa pande hizo na
ndiyo sababu ya kuufanya mvutano kuwa wa aina yake mpaka sasa, hasa ikizingatia vionjo walivyoviongeza msimu huu kama Kili Chat kipindi kinachorushwa EATV kila Alhamis saa
3:00 usiku.

"Kilimanjaro ni bia ya burudani zaidi kama mnavyofahamu, na kwa kutambua hilo ndiyo sababu ya kuzisapoti timu hizi, pia tunawapa fursa mashabiki ya kukaa pamoja na kutafakari mambo mbalimbali hata ya nje ya
timu zao,”alisema Kavishe.

Aidha Kavishe aliwataka mashabiki wa timu hizo kuvutana kikamilifu ili kuzipatia pesa klabu zao kwa ajili ya majukumu mbalimbali kwa kuwa kati ya mil 100, mil 80 ni ya kuvutana huku mil 20 zikiwa ni za dimbani mil 15 kwa mshindi na mil 5 kwa timu ambayo itakubali kichapo ikiwa kama kifuta
jasho.

Alitaja matokeo ya kuvutana mpaka sasa ambapo Yanga anaonekana kuongoza kuwa ni Oktoba 29 Simba sh 34,210,000 baada ya mashabiki wao 3360 kutuma meseji huku
Yanga sh 45,790,000 kutokana na mashabiki 3965.

Oktoba 28, Simba sh 35,250,000 baada ya mashabiki 3082 na Yanga sh 44,750,000 baada ya mashabiki wao 3,581, huku Oktoba 26 Simba akivuna sh 36,350,000 na Yanga sh 43,650,000, 

Huku Oktoba 25 Simba sh
37,260,000 na Yanga sh 42,740,000, Oktoba 24 Simba sh 38,400,000 na Yanga sh 41,600,000, huku akiwataka mashabiki wa timu hizo, kuhakikisha wanatumia vyema fursa hiyo ili kuzinufaisha timu zao.

Chapisha Maoni

 
Top