Tukio hilo lilitokea Oktoba 28,
mwaka huu ambapo Chid Benz alikuwa
akipelekwa Segerea huku mahabusu waliokuwemo ndani ya gari hilo wakitoa maneno ya kumkejeli pale alipokosa kiti na kulazimika kusimana.
Mmoja wa mahabusu alisikika akimzodoa Chid Benz kwa kumwambia: ‘Ustaa wako hukohuko, simama’ ambapo msanii huyo hakuleta ubishi,
alisimama na safari ya kuelekea Segerea ikaanza.
Chid Benz anadaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine yenye thamani ya Tsh. 38,638, Bangi zenye thamani ya Tsh. 1,720
pamoja na vifaa vya utumiaji wa kuvuta dawa hizo ambapo alikana mashitaka hayo na kurudishwa rumande hadi Novemba 11, mwaka huu kesi yake
itakapotajwa tena.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.