0
Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ameibuka na kumtaka msanii mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kukubaliana na matokeo
ya aliyekuwa mpenzi wake Vincent Kigos ‘Ray’ kwamba kwa sasa ana uhusiano na mtu mwingine.

Akizungumza na mwandishi wetu, Aunty Lulu alimtaka Johari kukubaliana na matokeo na aige mfano wake kwani aliachana na Bond Bin Sinan
ambaye kwa sasa ana mpenzi mwingine hivyo asimchukie Chuchu Hans anayetoka na Ray kwa sasa kwani kuachana ni jambo la kawaida katika
mapenzi hivyo hatakiwi kuwa na kinyongo.
“Mimi nimepitia kwenye maisha hayo ndiyo maana namshauri Johari akubaliane na matokeo kwamba Ray kwa sasa yupo na Chuchu Hans na
asiwe na kinyongo naye ampende na aongee naye vizuri tu kwani ndiyo maisha,” alisema Aunty
Lulu.

Chapisha Maoni

 
Top