Wananchi wa kijiji cha Mfuto katika Kata ya Ufulumo huko Wilayani Uyui, Tabora wamepatwa na mshituko na kuingiwa na hofu baada ya mti aina ya msufi, uliong'oka na kuanguka miaka
mitatu iliyopita, kuinuka na kusimama wima kama zamani.
Mti huo wenye kipeo cha futi mbili inaelezwa kuwa ulianguka kwa upepo mkali na kuungua kwa moto wakati wa kuandaa mashamba. Mtangazaji
wa TBC anasema kuwa mti huo ambao ulikuwa umeshambuliwa na mchwa, hivi majuzi ulionekana ukinyanyuka taratibu kana kwamba walikuwepo watu wanaunyanyua hadi uliposimama kama awali.
Mara baada ya kuenea kwa taarifa za kuinuka kwa mti huo, wananchi wengi walifika kwenye eneo husika na kuanza kugombea vipande vya mti huo,
ambapo kila mtu alitaka kupata walao gome aubsehemu yoyote ya mti huo ama hata udongo palipokuwa pamelala mti huo.
Afisa Mtendaji wa Kijii hicho, amesema kuwa Serikali ya Kijiji inaendelea kuwasiliana na Wazee wa kimila ili kupata maoni yao juu ya tukio hilo.
Chapisha Maoni