Aliyekuwa nahodha wa Simba, Hassan Isihaka,
ametamka kuwa kwa sasa hana timu ya kuichezea
na yupo nyumbani tu.
Isihaka ambaye alitengeneza ukuta imara akiwa
Simba akishirikiana na Mganda, Juuko Murshid,
ametemwa nje ya kikosi cha Simba ambacho
kimejichimbia mkoani Morogoro chini ya kocha
wake Mcameroon, Joseph Omog kikijiandaa na
msimu ujao wa ligi kuu.
Akizungumza kuhusiana naye, beki huyo
anayechipukia alisema kuwa mpaka sasa amekuwa
akikaa nyumbani tu kutokana na kutemwa na timu
yake hiyo ambapo hakuna timu yoyote ile
iliyomfuata kwa nia ya kumsajili.
“Nipo nyumbani tu, sina timu yoyote ya kuichezea
mara baada ya kutemwa na Simba ambapo mpaka
sasa hakuna timu yoyote ile ambayo imenifuata
kwa ajili ya kunisajili kwa msimu ujao.
“Sijajua hatma yangu itakuwaje msimu ujao kwa
sababu sina timu lakini naamini mambo yatakuja
kukaa vizuri kabla ya dirisha la usajili kufungwa,
timu zitakuja tu,” alisema Isihaka.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni