Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Newcastle,
Demba Ba ameanza mazoezi mepesi baada ya
kufanyiwa upasuaji na daktari bingwa kutoka
Ufaransa, Olivier Blinger ili kurekebisha mguu
wake uliovunjika siku chache zilizopita kwenye
mchezo wa Ligi Kuu ya China, CSL.
Ba aliumia vibaya baada ya kuchezewa vibaya na
nahodha wa klabu ya Shanghai SIPG, Sun Xiang
akiichezea klabu yake, Shanghai Shenhua
Nyota huyo wa kimataifa wa Senegal alihofiwa na
wengi kuwa huo ungekuwa mwisho wake wa
kucheza soka, lakini baada ya upasuaji wenye
mafanikio alieleza kuwa ataweza kupona na kurudi
uwanjani.
Sun Xiang ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa
China aliomba msamaha akieleza kuwa haikuwa
dhamira yake kumuumiza Ba.
Licha ya tukio hilo, Shenhua ilimfariji Ba kwa
ushindi wa mabao 2-1 kwa bao la ushindi la Fredy
Guarin.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni